Duration 2:47

TENGENEZENI KOZI ZA ELIMU ZA MUDA MFUPI ILI KUENDELEZA SEKTA YA BIASHARA NCHINI-SENYAMULE

7 watched
0
0
Published 15 Aug 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ametoa wito kwa Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE ) kutengeneza mfumo wa mafunzo ya kozi za muda mfupi ambazo zitalenga mahitaji ya wajasiriamali wadogo na kuwaongezea tija katika shughuli zao ili kuendelea kuufaharisha Mkoa wa Dodoma pamoja na kuendeleza sekta ya Elimu nchini. Wito huo umetolewa leo tarehe 14 Agosti,2023 chuoni hapo wakati akati akizindua Maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE )Kampasi ya Dodoma . Senyamule amewapongeza uongozi wa chuo kwa maandalizi ya mada ya mdahalo uliolenga kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za ajira hapa nchini. "Mada hii ni nzuri na imekuja kwa wakati muafaka kwani mwelekeo wa serikali ni kuandaa vijana wenye uwezo wa kujiajiri wenyewe. Niwaombe washiriki na wawakilishi wa taasisi mbalimbali kuyafanyia kazi uchambuzi na maoni yaliyotolewa kwenye mdahalo wa leo ili kufanikisha adhima ya serikali."amesema Senyamule Katika hatua nyingine,Mkuu wa Mkoa huyo ameeleza shughuli mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa ndani ya jiji katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu kuanzia shule za msingi mpya zinazoendelea kujengwa na kuboreshwa chini ya serikali ya awamu ya sita . "Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka miundombinu wezeshi ya elimu pamoja na kuongeza wafanyakazi ili watoto wa Kitanzania kupata maarifa sawa kwa wote "ameeleza Senyamule Kwa Upande Wake Makamu wa Chuo cha CBE Prf.Eda Tandi amesema Chuo kitaendelea kutoa Elimu kwa Wajasiriamali wengi zaidi kwani hadi sasa takribani wajasiliamali 600 wamefanikiwa kupata elimu .

Category

Show more

Comments - 0