Duration 3:39

MSANII NANDI AKUTANA NA RAIS DR.HUSSEIN ALI MWINYI IKULU ZNZ KWAAJILI YA TAMASHA LA NANDY FESTIVAL

37 watched
0
0
Published 23 Jul 2021

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amelipongeza Tamasha la “Nandy Festival” na kusema kwamba kufanyika kwa Tamasha hilo hapa nchini ni fursa ya kuutangaza utalii wa Zanzibar.Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokuwa akizungumza na wasanii wa Tamasha la “Nandy Festival” waliopo hapa Zanzibar wakiongozwa na mwanamuziki maarufu wa muziki wa kizazi kipya Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy.Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi aliupongeza utayari wa wasanii wa tamasha la “Nany Festival” kwa kuja Zanzibar na kufanya maonyesho hatua ambayo alisema ni faraja kwani maonyesho hayo yataendelea kuitangaza zaidi Zanzibar.Alieleza jinsi alivyofurahishwa na na hatua hiyo na kueleza kwamba ataendelea kushirikiana na wasanii hao na kila itakapowezekana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa tayari kutoa msaada utakaohitajikwa kwa lengo la kuitangaza Zanzibar na kuinua vipaji vya wasanii wake hasa ingazingatiwa kwamba tayari wasanii wa Tanzania Bara wamepiga hatua kubwa katika tasnia hiyo ya muziki.Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa licha ya kuwepo kwa matamasha mengi hapa Zanzibar lakini pia kufanyika kwa matamasha kama hayo ya “Nandy Festival” ni fursa ya kuyaendeleza matamasha kwani lengo ni kuwa na matamasha mengi ambapo ndani ya miezi yote 12 kukawepo matamasha na baada ya hapo kila mwezi ni vyema yawepo hata matamasha mawili.Rais Dk. Mwinyi aliongeza kuwa matamasha yana umuhimu mkubwa sana kwa sababu yanaleta watu kutoka nje na kusema kwamba muziki wa kizazi kipya nao unaweza kuleta watu wengi hapa nchini.Alisema kuwa muziki wa kizazi kipya unaweza kuleta wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo wageni wanaotakiwa Zanzibar si lazima watoke nje, kwani hata wageni wanaotoka katika maeneo ya ndani ya Tanzania ikiwemo Kigoma, Arusha, Mwanza pia ni wageni kwani nao watakuwa na manufaa ya kiuchumi.Alisisitiza kwamba ni vyema mashirikiano yakawepo kati ya wasanii hao na Serikali na kufanya matamasha mengi zaidi huku akisisitiza haja kwa Serikali kuwashika mkono wasanii sambamba na kushirikiana nao kikamilifu.Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba michezo nayo inaweza kuimarisha uchumi na kuutangaza utalii wa Zanzibar na kutolea mfano mashindano ya Marathon yaliyofanyika hivi karibuni hapa Zanzibar yatasaidia kuitangaza Zanzibar.Kwa upande wa muziki wa taarab, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa muziki huo hapa Zanzibar ni nyumbani hivyo, ni vyema hatua za makusudi zikachukuliwa katika kuuinua muziki huo kwani hapo siku za nyuma uliimarika zaidi ambapo palikuwepo hata mashindanio ya taarabu yaliyohusisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki hatua ambayo ilikuwa inanyanyua vipaji vya wasanii wa ndani na kuleta hamasa na kuinua utalii.Hivyo, alisema kwamba wakati umefika wa kurudisha matamasha ya muziki wa taarab na kumtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo ambae atakuwa kiungo katika kushughulikia masuala hayo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Rais Dk. Mwinyi alieleza utayari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kushirikiana na wasanii hao kwani kama unavyopendwa muziki wa kizazi kipya pia na muziki wa taarabu nao umekuwa na wapenzi wengi hapa nchini.Katika maelezo yake, Rais Dk. Miwnyi alisisitiza kwamba Serikali anayoiongoza itatumia njia ya kuwasaidia wasanii wa ndani ili waweze kuinua vipaji vyao.Alisema kwamba sanaa ni njia moja wapo ya kutoa ajira kwa vijana na kusema kwamba iwapo wasanii hao watasaidiana na wasanii wa Zanzibar hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa ajira vijana.Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi na shukurani kwa Nandy na wasanii wenzake kwa kufanya tamasha hapa Zanzibar na kukutana nao lei hii pamoja na hapo jana kukutana na mkewe Mama Mariam Mwinyi huku akitumia fursa hiyo kwa kumshukuru na kumpongeza Nandy na wasanii wengine kwa ushirikiano wao mkubwa katika Kampeni za uchaguzi za CCM zilizopita. “Nyinyi wasanii wa muziki wa kiziazi kipya mna uwezo mubwa wa kuvuta watu kwa hiyo wakati wa kampeni milikuwepo nyinyi na kina Aisha na wasanii kadha wa kadhaa kwa kweli tuna deni kwenu na tungependa kushirikiana katika masuala ya ajira na kuutangaza utalii wa Zanzibar”,alisema Dk. Mwinyi.Nae mwanamuziki nguli wa kizazi kipya hapa nchini Faustina Charles..,...........

Category

Show more

Comments - 0